
Neno la Leo
by Neno la Leo 255Season 4

Upendo wa Kweli Huheshimu Mipaka!
🎙️ Leo katika Neno la Leo tunatafakari 2 Samweli 13:10–14, sehemu nzito na yenye maumivu katika simulizi la familia ya Daudi. Amnoni anapokuwa peke yake na Tamari anajaribu kumlazimisha kutimiza tamaa yake. Tamari anakataa wazi. Anasema, “Usifanye jambo hili.” Lakini Amnoni hasikilizi. Anatumia nguvu zake na kumdhuru. Hapa Biblia inatuweka mbele ya ukweli ambao hatupaswi kuuficha kwa lugha nyepesi: Tamari alisema hapana. Amnoni hakuheshimu hapana yake. Huo haukuwa upendo. Upendo wa kweli haumfanyi mwingine kuwa chombo cha kutimiza tamaa zetu. Upendo haupimi tu kile tunachotaka sisi. Unaheshimu utu, sauti na mipaka ya mwingine. Ndiyo maana 1 Wakorintho 13:5 inasema kwamba upendo “hautafuti mambo yake.” Na tunapoisoma simulizi hii ni muhimu tusimwangalie Amnoni pekee. Tumwone Tamari pia. Hakusababisha alichofanyiwa. Alisema hapana. Alijaribu kumzuia. Responsibility ilikuwa ya Amnoni ambaye alichagua kupuuza sauti yake na kutumia nguvu dhidi yake. Hili ni muhimu sana hata katika mahusiano yetu leo. Kuwa katika relationship hakumpi mtu ownership ya mwili wa mwingine. Ndoa, uchumba au ukaribu hauondoi umuhimu wa kuheshimiana. Upendo wa kweli hauulizi tu, “Mimi nataka nini?” Unauliza pia, “Je, ninamheshimu huyu mtu?” Na kwa wale wanaobeba maumivu ya kudhulumiwa, simulizi la Tamari linatukumbusha kwamba aibu haipaswi kuwekwa juu ya aliyedhulumiwa. Responsibility ni ya aliyefanya ukatili. Upendo wa kweli unasikiliza. Upendo wa kweli haukulazimishi. Upendo wa kweli unaheshimu “hapana.” Karibu katika Neno la Leo tunapotafakari somo hili muhimu na kuomba Mungu atufundishe kuwapenda wengine kwa heshima, utu na moyo usiotafuta faida yake mwenyewe.
Usilishe Tamaa Isiyofaa Moyoni
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 13:1–2 tunaingia katika sehemu ngumu na yenye huzuni katika familia ya Daudi. Tunamkuta Amnoni akianza kuwa na tamaa isiyofaa kwa Tamari, dada yake wa kambo. Lakini kuna jambo muhimu ambalo maandiko yanatuonyesha kabla hata hatujafika kwenye kile kitakachotokea baadaye. Amnoni anaendelea kuibeba na kuilisha tamaa hiyo moyoni mpaka inamtesa. Na hapa tunahitaji kutofautisha mambo mawili. Wazo linalopita kichwani na uamuzi wa kulipa nafasi ni vitu viwili tofauti. Hatuchagui kila wazo linalotokea akilini. Hatuchagui kila temptation inayojitokeza. Lakini tuna responsibility juu ya kile tunachokiruhusu kikae, kikue na kuanza kutawala mawazo yetu. Yakobo 1:14–15 anatupa picha ya jinsi tamaa inavyoweza kukua mpaka kuzaa dhambi. Na hapo ndipo simulizi la Amnoni linakuwa onyo kubwa kwetu. Tatizo lake halikuanza siku alipomdhuru Tamari. Lilikuwa limeanza moyoni. Kabla ya tendo kulikuwa na tamaa. Kabla ya mpango kulikuwa na mawazo yaliyokuwa yakipewa nafasi. Na kabla wengine hawajaona tatizo, tayari kulikuwa na vita ambavyo Amnoni alikuwa akivipoteza ndani yake. Hilo linatuuliza swali muhimu: Ni kitu gani ninachokilisha moyoni ambacho najua hakipaswi kukua? Huenda si tamaa ya kingono. Inaweza kuwa wivu. Hasira. Kisasi. Tamaa ya mali. Kiburi. Kutamani maisha ya mtu mwingine. Au fantasy ambayo tunajua inatupeleka mahali pasipo sahihi. Mara nyingi tunataka kupambana na dhambi ikiwa tayari imekuwa kubwa. Lakini hekima ni kuikabili ikiwa bado ni mbegu. Usisubiri wazo baya ligeuke kuwa tendo ndipo uanze kupigana nalo. Na hapa kuna distinction muhimu pia. Kujaribiwa hakukufanyi moja kwa moja kuwa mtu mbaya. Wazo baya kujitokeza akilini halimaanishi tayari umelitenda. Swali ni: Utafanya nini nalo? Utalikataa au utalirudia tena na tena? Utalileta mbele za Mungu au utalificha na kulikuza? Utalikata mapema au utasubiri mpaka likuanze kukutawala? Wafilipi 4:8 inatukumbusha kuelekeza mawazo yetu katika yaliyo ya kweli, yenye heshima na yaliyo safi. Kwa sababu kile tunachoruhusu kikae akilini kinaweza kuanza kutengeneza kile tunachotamani. Na kile tunachotamani kinaweza kuanza kuongoza kile tunachofanya. Kwa hiyo usidharau vita vinavyoendelea moyoni. Kuna vita ambavyo ni rahisi zaidi kuvishinda vikiwa bado ni mawazo kuliko baada ya kuwa matendo. Usilishe kile ambacho hutaki kikuze ndani yako. Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Mungu Bado Anaweza Kuandika Sura Mpya!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:24–25 tunafika katika sehemu tofauti kabisa ya simulizi la Daudi. Tumemwona akikosea vibaya. Tumemwona akikubali dhambi yake. Tumemwona akisamehewa lakini akikabiliana na consequences. Tumemwona akiomba. Tumemwona akilia. Na jana tulimwona akiinuka tena. Leo Biblia inatuonyesha kwamba hadithi haikuishia pale. Daudi anamfariji Bathsheba. Baadaye wanapata mtoto mwingine: Sulemani. Kisha Biblia inasema maneno machache lakini yenye uzito mkubwa: “Bwana akampenda.” Hapa tunahitaji kuwa careful tusikimbilie kuifanya sehemu hii kana kwamba yaliyopita hayakuwa muhimu. Maumivu hayajafutwa. Dhambi ya Daudi haijaitwa kitu kizuri. Consequences hazijafanywa kana kwamba hazikutokea. Lakini Mungu bado anaandika. Na hiyo ndiyo neema. Wakati mwingine baada ya kufanya kosa kubwa tunaanza kuamini kwamba tumefuta kila jambo zuri ambalo lingeweza kutokea katika maisha yetu. Tunasema: “Niliharibu.” Na labda ni kweli. Lakini kisha tunaongeza conclusion ambayo Mungu hajaitoa: “Kwa hiyo hakuna future tena.” Hapo ndipo tunahitaji kuwa makini. Kukubali kosa lako ni toba. Lakini kuamua kwamba Mungu hawezi kufanya chochote tena na maisha yako si lazima iwe toba. Wakati mwingine ni sisi wenyewe kuweka full stop mahali ambapo Mungu bado anaandika. Sulemani anatokea katika historia ambayo haikuwa clean. Na baadaye huyu Sulemani atakuwa sehemu muhimu sana katika historia ya Israeli. Hilo halifanyi kosa la Daudi kuwa sawa. Linatufundisha kitu tofauti: Mungu anaweza kuleta kusudi hata kutoka katika maisha yaliyovunjika. Neema haibadilishi jana kana kwamba haikutokea. Lakini neema inaweza kubadilisha kile jana itamaanisha kwa kesho yako. Kosa linaweza kuwa sehemu ya historia yako bila kuwa identity yako yote. Hasara inaweza kuwa chapter bila kuwa mwisho wa kitabu. Failure inaweza kukufundisha bila kupewa mamlaka ya kuamua kila kitu ambacho bado unaweza kuwa. Kwa hiyo kama kuna sehemu ya maisha yako ambayo ukiitazama unasema: “Niliharibu hapa.” Kubali kilichotokea. Tubu pale unapohitaji kutubu. Rekebisha unachoweza kurekebisha. Jifunze. Lakini baada ya hapo, endelea kutembea na Mungu. Kwa sababu consequences zinaweza kubaki lakini hazina mamlaka ya kuamua kwamba hakuna future. Makosa ya jana hayafuti kesho ambayo Mungu bado anaandika. Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Baada ya Siku Ngumu, Unaweza Kuinuka Tena
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:20 tunakutana na Daudi baada ya kupokea jibu ambalo hakulitaka. Jana tulimwona akiwa chini, akifunga na kumwomba Mungu kwa ajili ya mtoto wake. Leo habari inafika: Mtoto amekufa. Watumishi wa Daudi wanaogopa hata kumwambia. Wanafikiri kama alikuwa katika hali ile mtoto akiwa hai, atakuwaje akigundua kwamba amekufa? Lakini Daudi anaposikia habari hiyo anafanya jambo ambalo hawakutarajia. Anaondoka chini. Anaoga. Anabadilisha mavazi. Anaingia katika nyumba ya Bwana na kuabudu. Hii haimaanishi Daudi hakuhuzunika. Haimaanishi kilichotokea hakikuwa painful. Na wala Biblia haitufundishi kwamba mtu anayepitia grief anapaswa kuharakishwa “aendelee na maisha.” Lakini Daudi anatufundisha kwamba kuna tofauti kati ya kuomboleza kile kilichotokea na kuacha maisha yetu yabaki pale milele. Kuna wakati Daudi aliomba hali ibadilike. Lakini sasa anakutana na jambo ambalo hawezi kulibadilisha. Na anapaswa kujifunza kuendelea kutembea na Mungu katika reality ambayo hakuitaka. Hapo ndipo reflection hii inatugusa. Kuna mambo ambayo tumeyaombea sana lakini hayakwenda tulivyotarajia. Kuna relationship ambayo haikurudi. Kuna mlango ambao haukufunguka. Kuna opportunity iliyopita. Kuna ndoto iliyobadilika. Na kuna hasara ambazo hatuwezi kuzireverse. Katika nyakati kama hizo, swali linabadilika. Mwanzoni tuliuliza: “Bwana, unaweza kubadilisha hili?” Lakini baada ya kile kisichoweza kubadilishwa kutokea, huenda sala yetu ikawa: “Bwana, sasa nifundishe jinsi ya kuendelea nawe kutoka hapa.” Na kuna kitu kingine kizuri sana katika mstari huu. Daudi anaabudu. Hakuabudu kwa sababu amepata jibu alilotaka. Anaabudu wakati jibu limekuwa tofauti kabisa na alivyotamani. Hiyo ni aina ngumu sana ya worship. Ni kumwambia Mungu: “Sielewi kila kilichotokea. Ninaumia. Huenda bado nina maswali. Lakini bado wewe ni Mungu wangu.” Kuinuka tena hakumaanishi umesahau. Hakumaanishi haukuumia. Hakumaanishi kwamba kile ulichopoteza hakikuwa muhimu. Kuinuka kunamaanisha maumivu hayatapewa mamlaka ya kutangaza kwamba safari yako imeishia hapo. Unaweza kuomboleza na bado kuendelea. Unaweza kuwa na maswali na bado kuabudu. Unaweza kubeba kumbukumbu ya kile kilichotokea na bado kumruhusu Mungu akupeleke kwenye hatua inayofuata. Na baada ya siku ngumu sana, kwa neema ya Mungu: Unaweza kuinuka tena. Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Omba Hata Kama Hujui Mungu Atajibu Vipi!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:16–17 tunamwona Daudi katika sehemu tofauti kabisa na jana. Jana alisimama mbele ya Nathani na kukubali: “Nimemkosea Bwana.” Leo yuko chini mbele za Mungu akiomba. Mtoto wake anaumwa sana. Daudi anafunga, anaingia ndani na kulala chini usiku kucha akimtafuta Mungu. Na hapa kuna jambo la kuvutia. Daudi tayari amesikia kile Nathani alichosema. Hajui kama hali itabadilika. Lakini bado anaomba. Hapo tunajifunza jambo muhimu kuhusu maombi. Wakati mwingine tunaingia katika maombi tukijua kabisa tunachotamani. Tunataka uponyaji. Tunataka mlango ufunguke. Tunataka relationship irejeshwe. Tunataka kazi, mtoto, breakthrough au hali fulani ibadilike. Lakini hatujui Mungu atajibu vipi. Je, bado tunaomba? Daudi anatufundisha ndiyo. Maombi si lazima yaanze na uhakika kuhusu outcome. Yanaweza kuanza na uhakika kuhusu Mungu tunayemwendea. Daudi hakujua Mungu angebadilisha hali au la. Lakini alijua bado anaweza kuingia mbele zake na kumwambia kile moyo wake unatamani. Na Yesu mwenyewe kule Gethsemane anatupa picha yenye nguvu zaidi. Alimweleza Baba kile alichotamani lakini akasema: “Si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo wewe.” Hiyo si imani dhaifu. Hiyo ni imani iliyokomaa. Imani inayoweza kuomba kwa ujasiri bila kujaribu kumdhibiti Mungu. Imani inayoweza kusema: “Bwana, hiki ndicho ninachotamani. Hiki ndicho ninachokuomba. Lakini kama jibu lako litakuwa tofauti na nilivyotarajia, bado nitakuamini.” Na hiyo si rahisi. Kwa sababu wakati mwingine hatutaki tu Mungu asikie maombi yetu. Tunataka atupe jibu tulilokwisha kulichagua. Lakini maombi yanatualika kufanya jambo la ndani zaidi: Kumkabidhi Mungu si ombi letu tu bali pia matokeo yake. Kwa hiyo kuna jambo ambalo hujui litamalizikaje? Usiache kuomba kwa sababu huna uhakika wa jibu. Mweleze Mungu unachotamani. Lia mbele zake ikiwa unaumia. Omba kwa imani. Lakini pamoja na ombi lako, mpe pia moyo wako. Kwa sababu imani si kusema, “Najua Mungu atafanya exactly ninachotaka.” Wakati mwingine imani ni kusema: “Sijui Mungu atajibu vipi, lakini najua bado ninaweza kumwamini.” Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Ukikosea, Usijifiche. Rudi kwa Mungu!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:13–14 tunakutana na moja ya moments nzito zaidi katika maisha ya Daudi. Nabii Nathani amesimama mbele yake na kumwambia wazi: “Wewe ndiye mtu huyo.” Daudi sasa hana mahali pa kujificha. Angeweza kujitetea. Angeweza kutoa sababu. Angeweza kutumia mamlaka yake kama mfalme kumyamazisha Nathani. Lakini Daudi anasema: “Nimemkosea Bwana.” Hakuna excuse. Hakuna blame shifting. Anakubali. Na Nathani anamjibu kwamba Bwana ameiondoa dhambi yake. Hapo tunaona uzuri mkubwa wa neema ya Mungu. Baada ya yote ambayo Daudi amefanya, mlango wa toba bado uko wazi. Mungu yuko tayari kumsamehe mtu anayekuja kwake kwa moyo wa kweli. Lakini ndipo tunakutana na ukweli mwingine ambao wakati mwingine ni mgumu kuukubali: Msamaha hauondoi kila matokeo. Daudi amesamehewa lakini baadhi ya consequences za uchaguzi wake bado zitagusa maisha na familia yake. Na hapa ndipo tunahitaji kutofautisha mambo mawili. Kusamehewa na Mungu si sawa na kufutwa kwa consequences zote za uchaguzi wetu. Unaweza kusamehewa lakini trust ikahitaji kujengwa tena. Unaweza kusamehewa lakini ukahitaji kuomba msamaha kwa mtu uliyemuumiza. Unaweza kusamehewa lakini ukahitaji kurekebisha uharibifu uliosababisha. Unaweza kusamehewa lakini baadhi ya matokeo yakahitaji muda kuyapitia. Hiyo haimaanishi neema ya Mungu imeshindwa. Ina maana neema haifanyi dhambi kuwa jambo dogo. Na hapa ndipo Daudi anatufundisha jambo muhimu. Anapokabiliwa na dhambi yake, haanzi kwa kujitetea. Anasema: “Nimemkosea Bwana.” Huenda moja ya dalili za toba ya kweli ni pale tunapoacha kuuliza, “Nitaelezaje kwa nini nilifanya hivi?” na kuanza kusema, “Nilifanya vibaya. Bwana nisamehe na unionyeshe ninachopaswa kurekebisha.” 1 Yohana 1:9 inatukumbusha kwamba tunapoziungama dhambi zetu, Mungu ni mwaminifu na wa haki kutusamehe na kutusafisha. Lakini neema hiyo haituiti kukimbia responsibility. Inatupa nguvu ya kuikabili. Kwa hiyo kama umekosea, usikimbie mbali na Mungu. Rudi. Ungama. Tubu. Kubali kusahihishwa. Rekebisha kile unachoweza kurekebisha. Na pale ambapo consequences haziwezi kubadilishwa, mwombe Mungu akupe neema ya kuzipitia bila kurudi kwenye dhambi ileile. Kwa sababu habari njema si kwamba makosa yetu hayana matokeo. Habari njema ni kwamba hata baada ya makosa yetu, Mungu anaweza kutusamehe, kutubadilisha na kuendelea kufanya kazi ndani yetu. Msamaha hauondoi kila matokeo lakini dhambi yako si lazima iwe neno la mwisho juu ya maisha yako. Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨Season 3

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:23–26 na 31:1–4 tunafunga mwezi wetu na wakati huohuo tunafika mwisho wa safari yetu kupitia kitabu cha 1 Samweli. Na Biblia inatuacha na picha mbili tofauti sana: Daudi na Sauli. Daudi anatoka katika kipindi kigumu sana kule Ziklagi. Ameona mji wake ukiteketea. Amelia mpaka hana nguvu. Watu wake wametaka kumpiga mawe. Lakini Daudi akajitia nguvu katika Bwana, akamwuliza Mungu hatua inayofuata na mwisho akapata ushindi. Baada ya ushindi, baadhi ya watu wake wanataka kujichukulia nyara na kuwanyima wale waliokuwa wamechoka na kubaki nyuma. Lakini Daudi anasema kwa maana: “Msifanye hivyo na kile Bwana alichotupa.” Hapo tunaona kitu kuhusu moyo wa Daudi. Baada ya ushindi hakusema, “Angalieni nilichofanya.” Alikumbuka: “Bwana ndiye aliyetupa.” Na hata kile alichopokea hakukishikilia kwa ajili yake mwenyewe. Akagawa na wengine. Lakini tunapofungua sura ya mwisho ya 1 Samweli, tunakutana na picha nyingine. Sauli anafika mwisho wa safari yake. Na mwisho wake ni wa kusikitisha sana kwa sababu Sauli alianza vizuri. Alichaguliwa. Akapakwa mafuta. Roho wa Mungu akaja juu yake. Akapewa nafasi kubwa ya kuliongoza taifa. Lakini hatua kwa hatua moyo wake ukaanza kubadilika. Kutokutii. Hofu ya watu. Wivu. Hasira. Kulinda nafasi yake. Mpaka Daudi, mtu ambaye angeweza kuwa msaada kwake, akawa mtu ambaye Sauli alitumia miaka mingi akimfukuza. Halafu tunamtazama Daudi. Na hapa tunahitaji kukumbuka: Daudi hakuwa perfect. Tumemwona akiogopa. Tumemwona akichoka. Tumemwona akiwa karibu kulipiza kisasi. Tumemwona akifanya maamuzi akiwa chini ya pressure. Tumemwona akilia mpaka hana nguvu tena za kulia. Kwa hiyo tofauti kati ya Daudi na Sauli haikuwa kwamba mmoja hakuwahi kukosea. Tofauti muhimu tunayokutana nayo tena na tena ni hii: Daudi aliendelea kurudi kwa Mungu. Akichanganyikiwa, anamwuliza Mungu. Akidhoofika, anajitia nguvu katika Bwana. Akisahihishwa na Abigaili, anakubali kusahihishwa. Akipata ushindi, anakumbuka aliyempa ushindi. “Bwana ndiye aliyetupa.” Na hapo tunarudi kwenye somo tuliloanza nalo mwezi huu: Mungu anaangalia moyo. Unaweza kuwa na karama. Unaweza kuwa na nafasi. Unaweza kuwa na calling. Unaweza kuanza vizuri sana. Lakini swali muhimu zaidi ni: Moyo wako unaendelea kwenda upande gani? Paulo alipofika karibu na mwisho wa safari yake hakusema tu, “Nilianza vizuri.” Alisema: “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda.” Mwendo nimeumaliza. Na tunapofunga mwezi, labda hilo ndilo swali tunalopaswa kubaki nalo: Baada ya yote niliyopitia mwezi huu, moyo wangu uko wapi? Je, bado ninamtafuta Mungu? Je, nimekuwa karibu naye zaidi au nimeanza kwenda mbali? Kuna hasira ninayobeba? Kuna wivu? Kuna kutokusamehe? Kuna jambo Mungu amekuwa akiniambia niliachilie lakini bado nimelishikilia? Kuna sehemu ninahitaji kurudi kwake? Kwa sababu safari ya Sauli na Daudi inatuachia ukumbusho mzito: Sio tu jinsi unavyoanza. Ni jinsi unavyomaliza. Na kwa neema ya Mungu, tusitafute tu kuanza vizuri. Tuombe tumalize vizuri. 🙏📖 Karibu tusikilize, tutafakari na tufunge mwezi pamoja katika Neno la Leo. 
Mungu Anaweza Kukurejeshea Ulichofikiri Kimepotea!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:8, 18–19 tunaendelea na Daudi baada ya moja ya siku ngumu zaidi katika maisha yake. Jana tulimwacha Ziklagi ikiwa imechomwa moto. Familia zimechukuliwa mateka. Watu wake wamevunjika moyo kiasi cha kutaka kumpiga mawe. Daudi akalia mpaka hakuwa na nguvu tena za kulia. Lakini Biblia ikasema: “Daudi akajitia nguvu katika Bwana Mungu wake.” Leo tunaona jambo muhimu sana. Baada ya kupata nguvu, Daudi hafanyi maamuzi kwa hasira. Hakimbilii kuwafukuza Waamaleki kwa sababu tu anajua kupigana. Anafanya kitu ambacho tumemwona akikifanya kabla: Anamwuliza Mungu. “Je, nikiwafuata nitawapata?” Hili ni muhimu. Maumivu hayakumfanya Daudi aache kutafuta mwongozo wa Mungu. Hata baada ya kila kitu kilichotokea, bado anarudi kwenye swali lilelile: “Bwana, nifanye nini sasa?” Mungu anamwambia afuatilie. Daudi anachukua hatua na mwisho Biblia inasema: “Daudi akavipata vyote.” Jana alikuwa analia akitazama kile alichofikiri amepoteza. Leo anashuhudia kurejeshwa kwake. Lakini hapa tunahitaji kuelewa ujumbe huu vizuri. Biblia haitufundishi kwamba kila kitu tunachopoteza katika maisha lazima kirudi exactly katika namna ileile. Kuna hasara ambazo ni halisi. Kuna milango inayofungwa. Kuna vipindi vinavyokwisha na kuna mambo ambayo hayatakuwa tena kama yalivyokuwa. Lakini Ziklagi inatufundisha jambo jingine lenye nguvu: Hasara haimaanishi kwamba Mungu amemaliza hadithi yako. Daudi alipokuwa analia hakujua kwamba recovery ilikuwa mbele yake. Na huenda nasi tunafanya kosa la kuweka full stop katika sehemu ambayo Mungu ameweka comma. Tunasema, “Imeisha.” Mungu bado anaandika. Tunasema, “Hakuna kitakachotokea tena.” Lakini hatujaiona kesho. Restoration yako inaweza isifanane exactly na kile kilichopotea. Inaweza kuwa Mungu kurejesha nafasi. Inaweza kuwa uponyaji wa moyo. Inaweza kuwa direction mpya. Inaweza kuwa hekima uliyoipata kupitia kile ulichopitia au mwanzo mpya ambao hukuwahi kuufikiria. Jambo muhimu ni hili: usifanye maumivu ya jana kuwa unabii wa kesho yako. Angalia journey ya Daudi: Alilia. Akajitia nguvu katika Bwana. Akamwuliza Mungu. Akasikia direction. Kisha akasimama na kwenda. Hiyo ndiyo faith journey. Kuna wakati wa kulia. Kuna wakati wa kujitia nguvu katika Mungu. Kuna wakati wa kuuliza, “Bwana, hatua inayofuata ni ipi?” Halafu kuna wakati wa kusimama na kwenda. Kwa hiyo kama leo unasimama mbele ya Ziklagi yako na kuona majivu ya kitu ulichokipenda, usikimbilie kuamua kwamba kila kitu kimekwisha. Usiweke full stop mahali Mungu bado anaandika. Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Unaweza Kulia na Bado Ukawa na Imani!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:3–6 tunakutana na moja ya siku nzito zaidi katika maisha ya Daudi. Daudi na watu wake wanarudi Ziklagi wakitarajia kurudi nyumbani. Lakini wanapofika, wanakuta mji umechomwa moto na familia zao zimechukuliwa mateka. Biblia inasema: “Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakapaza sauti zao wakalia hata walipokuwa hawana nguvu tena za kulia.” Hawa ni mashujaa. Wamepitia vita. Wameishi jangwani. Wamekabiliana na hatari nyingi. Lakini leo wanalia. Na Daudi analia pamoja nao. Huyu ni Daudi aliyesimama mbele ya Goliathi. Huyu ni Daudi aliyepakwa mafuta kuwa mfalme. Huyu ni Daudi ambaye tumemfuatilia tukiona imani na ujasiri wake. Lakini leo hana motivational speech. Ana machozi. Na hapo tunajifunza jambo muhimu: imani haimaanishi kwamba hutawahi kuvunjika moyo. Kuna maumivu ambayo huwezi kuyafunika kwa maneno mazuri. Kuna siku ambazo jambo la kiroho zaidi unaloweza kufanya ni kuacha kujifanya uko sawa na kumwambia Mungu: “Bwana, hili limeniumiza.” Lakini simulizi la Daudi halimaliziki kwenye machozi. Baada ya kulia mpaka hana nguvu tena, hali inakuwa mbaya zaidi. Watu wake wenyewe wanamgeukia. Wakiwa katika uchungu wanaanza hata kuzungumza kuhusu kumpiga mawe. Fikiria Daudi hapo. Nyumbani hakuna. Familia haipo. Watu aliowaongoza wanamlaumu. Yonathani hayupo. Samueli hayupo. Hakuna mtu wa kumshika mkono na kumwambia, “Daudi, endelea.” Ndipo Biblia inasema: “Lakini Daudi akajitia nguvu katika Bwana Mungu wake.” Hapo ndipo moyo wa episode yetu ulipo. Kuna nyakati Mungu atatumia Yonathani kukutia nguvu. Tuliona hilo katika 1 Samweli 23:16. Lakini kuna siku Yonathani hatakuwepo. Na katika siku hizo, tunahitaji kujifunza kwenda kwa Mungu wenyewe. Si kujifanya hatuumii. Si kukataa machozi. Bali kusema: “Bwana, nimeumia. Nimechoka. Sina nguvu tena. Lakini bado wewe ni Mungu wangu. Nitie nguvu.” Hii ndiyo imani inayokomaa. Imani ambayo inaweza kulia mbele za Mungu na bado kumshikilia Mungu. Kwa hiyo kama unapitia siku nzito, usijione kwamba umepoteza imani kwa sababu umelia. Lia ikiwa unaumia. Mweleze Mungu ukweli wa moyo wako. Lakini usiishie kwenye machozi. Rudi kwa Mungu ambaye anaweza kukupa nguvu ya kusimama tena. Kwa sababu unaweza kulia na bado ukawa na imani. Machozi si mwisho wa hadithi. Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Usifanye Maamuzi Makubwa Ukiwa Umechoka na Kuogopa!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 27:1 tunakutana na Daudi katika hali ambayo huenda wengi wetu tunaifahamu. Jana alikuwa amesimama imara katika imani. Alikuwa na nafasi nyingine ya kumuua Sauli lakini akakataa. Alikuwa tayari kumwachia Mungu matokeo. Lakini leo tunamsikia Daudi akisema moyoni mwake: “Siku moja nitaangamia kwa mkono wa Sauli.” Ngoja kidogo. Huyu si Daudi aliyemshinda Goliathi? Si huyu ambaye Mungu amemwokoa kutoka kwa Sauli tena na tena? Si huyu ambaye tayari amepakwa mafuta kwa ajili ya kusudi kubwa? Ndiyo. Lakini Daudi amechoka. Amekimbia kwa muda mrefu. Leo yuko pangoni, kesho jangwani na kesho kutwa sehemu nyingine. Ameishi muda mrefu chini ya pressure ya kujiuliza Sauli atampata lini. Na sasa uchovu unaanza kuzungumza kuhusu kesho yake. Hapo ndipo tunapata somo muhimu sana. Wakati mwingine tunapokuwa tumechoka, hofu huanza kutafsiri maisha yetu. Tunaanza kuona kama haiwezekani kile ambacho jana tuliamini kinawezekana. Baada ya kuomba muda mrefu tunasema, “Labda Mungu hatajibu.” Baada ya kusubiri tunasema, “Labda haitabadilika.” Baada ya kupambana kwa muda mrefu tunasema, “Labda niache tu.” Lakini hisia ya leo si lazima iwe ukweli kuhusu kesho. Kumbuka historia ya Daudi. Sauli alikuwa amemtafuta mara nyingi lakini Mungu alikuwa amemhifadhi. Kilichobadilika katika mstari huu si uaminifu wa Mungu. Daudi amechoka. Na hilo linatufundisha kuwa makini sana na maamuzi makubwa tunapokuwa tumechoka, tumeumia au tunaogopa. Haimaanishi tusifanye maamuzi magumu. Wakati mwingine mabadiliko yanahitajika. Lakini kabla ya kufanya uamuzi mkubwa, huenda tunahitaji kwanza kupumzika, kuomba, kutafuta ushauri wenye hekima na kupata perspective tena. Usiache uchovu wa muda mfupi ukushawishi kwamba Mungu amefuta kila alichokuwa akifanya katika maisha yako. Kabla hujasema, “Imeisha,” kumbuka jinsi Mungu alivyokubeba mpaka hapa. Kabla hujasema, “Sitaweza,” jiulize kama ni ukweli unaozungumza au uchovu. Na kabla hujabadilisha kila kitu kwa sababu ya hofu ya leo, rudi mbele za Mungu. Kwa sababu wakati mwingine unachohitaji si mpango mpya. Unahitaji nguvu mpya. Usiruhusu uchovu wa leo uamue kesho yako. Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨