

Omba Hata Kama Hujui Mungu Atajibu Vipi!
Episode notes
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 12:16–17 tunamwona Daudi katika sehemu tofauti kabisa na jana.
Jana alisimama mbele ya Nathani na kukubali:
“Nimemkosea Bwana.”
Leo yuko chini mbele za Mungu akiomba.
Mtoto wake anaumwa sana. Daudi anafunga, anaingia ndani na kulala chini usiku kucha akimtafuta Mungu.
Na hapa kuna jambo la kuvutia.
Daudi tayari amesikia kile Nathani alichosema. Hajui kama hali itabadilika.
Lakini bado anaomba.
Hapo tunajifunza jambo muhimu kuhusu maombi.
Wakati mwingine tunaingia katika maombi tukijua kabisa tunachotamani. Tunataka uponyaji. Tunataka mlango ufunguke. Tunataka relationship irejeshwe. Tunataka kazi, mtoto, breakthrough au hali fulani ibadilike.
Lakini hatujui Mungu atajibu vipi.
Je, bado tunaomba?
Daudi anatufundisha ndiyo.
Maombi si lazima yaanze na uhakika kuhusu outcome. Yanaweza kuanza na uhakika kuhusu Mungu tunayemwendea.
Daudi hakujua Mungu angebadilisha hali au la. Lakini alijua bado anaweza kuingia mbele zake na kumwambia kile moyo wake unatamani.
Na Yesu mwenyewe kule Gethsemane anatupa picha yenye nguvu zaidi. Alimweleza Baba kile alichotamani lakini akasema:
“Si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo wewe.”
Hiyo si imani dhaifu.
Hiyo ni imani iliyokomaa.
Imani inayoweza kuomba kwa ujasiri bila kujaribu kumdhibiti Mungu.
Imani inayoweza kusema:
“Bwana, hiki ndicho ninachotamani. Hiki ndicho ninachokuomba. Lakini kama jibu lako litakuwa tofauti na nilivyotarajia, bado nitakuamini.”
Na hiyo si rahisi.
Kwa sababu wakati mwingine hatutaki tu Mungu asikie maombi yetu. Tunataka atupe jibu tulilokwisha kulichagua.
Lakini maombi yanatualika kufanya jambo la ndani zaidi:
Kumkabidhi Mungu si ombi letu tu bali pia matokeo yake.
Kwa hiyo kuna jambo ambalo hujui litamalizikaje?
Usiache kuomba kwa sababu huna uhakika wa jibu.
Mweleze Mungu unachotamani.
Lia mbele zake ikiwa unaumia.
Omba kwa imani.
Lakini pamoja na ombi lako, mpe pia moyo wako.
Kwa sababu imani si kusema, “Najua Mungu atafanya exactly ninachotaka.”
Wakati mwingine imani ni kusema:
“Sijui Mungu atajibu vipi, lakini najua bado ninaweza kumwamini.”
Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨