

Baada ya Siku Ngumu, Unaweza Kuinuka Tena
Episode notes
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 12:20 tunakutana na Daudi baada ya kupokea jibu ambalo hakulitaka.
Jana tulimwona akiwa chini, akifunga na kumwomba Mungu kwa ajili ya mtoto wake.
Leo habari inafika:
Mtoto amekufa.
Watumishi wa Daudi wanaogopa hata kumwambia. Wanafikiri kama alikuwa katika hali ile mtoto akiwa hai, atakuwaje akigundua kwamba amekufa?
Lakini Daudi anaposikia habari hiyo anafanya jambo ambalo hawakutarajia.
Anaondoka chini. Anaoga. Anabadilisha mavazi. Anaingia katika nyumba ya Bwana na kuabudu.
Hii haimaanishi Daudi hakuhuzunika.
Haimaanishi kilichotokea hakikuwa painful.
Na wala Biblia haitufundishi kwamba mtu anayepitia grief anapaswa kuharakishwa “aendelee na maisha.”
Lakini Daudi anatufundisha kwamba kuna tofauti kati ya kuomboleza kile kilichotokea na kuacha maisha yetu yabaki pale milele.
Kuna wakati Daudi aliomba hali ibadilike.
Lakini sasa anakutana na jambo ambalo hawezi kulibadilisha.
Na anapaswa kujifunza kuendelea kutembea na Mungu katika reality ambayo hakuitaka.
Hapo ndipo reflection hii inatugusa.
Kuna mambo ambayo tumeyaombea sana lakini hayakwenda tulivyotarajia.
Kuna relationship ambayo haikurudi.
Kuna mlango ambao haukufunguka.
Kuna opportunity iliyopita.
Kuna ndoto iliyobadilika.
Na kuna hasara ambazo hatuwezi kuzireverse.
Katika nyakati kama hizo, swali linabadilika.
Mwanzoni tuliuliza:
“Bwana, unaweza kubadilisha hili?”
Lakini baada ya kile kisichoweza kubadilishwa kutokea, huenda sala yetu ikawa:
“Bwana, sasa nifundishe jinsi ya kuendelea nawe kutoka hapa.”
Na kuna kitu kingine kizuri sana katika mstari huu.
Daudi anaabudu.
Hakuabudu kwa sababu amepata jibu alilotaka.
Anaabudu wakati jibu limekuwa tofauti kabisa na alivyotamani.
Hiyo ni aina ngumu sana ya worship.
Ni kumwambia Mungu:
“Sielewi kila kilichotokea. Ninaumia. Huenda bado nina maswali. Lakini bado wewe ni Mungu wangu.”
Kuinuka tena hakumaanishi umesahau.
Hakumaanishi haukuumia.
Hakumaanishi kwamba kile ulichopoteza hakikuwa muhimu.
Kuinuka kunamaanisha maumivu hayatapewa mamlaka ya kutangaza kwamba safari yako imeishia hapo.
Unaweza kuomboleza na bado kuendelea.
Unaweza kuwa na maswali na bado kuabudu.
Unaweza kubeba kumbukumbu ya kile kilichotokea na bado kumruhusu Mungu akupeleke kwenye hatua inayofuata.
Na baada ya siku ngumu sana, kwa neema ya Mungu:
Unaweza kuinuka tena.
Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨