Wanangu podcast

Wanangu podcast

by Goodluck Joseph

Episode 78 | Falsafa za Yuri Boyka

Host anatukumbusha umuhimu wa kugeuza hasi kuwa chanya katika kila gumu tunalopitia huku akitoa mfano kutoka katika moja ya filamu maarufu za sanaa za mapigano (Martial arts) inayoitwa Undisputed III: Redemption. Song of the week: Dilly Darling by Nikita Kering.

Episode 77 | Mwanajua by Dizasta Vina (Uchambuzi)

Baada ya episode ya 75 kuchambua wimbo wa “Mbuzi” wa Dizasta Vina, watazamaji wa Wanangu podcast Youtube wameomba uchambuzi wa wimbo wake wa “Mwanajua” kutoka katika album yake ya The Verteller (2020). Episode hii imekuja kutuliza kiu yao.

Episode 76 | Malezi bora ni yapi?

Katika episode hii, host ana-share mawazo yake juu ya malezi, ikichangiwa na mazungumzo aliyowahikufanya na watu mbali mbali katika maisha yake ya kila siku pamoja na uzoefu wake binafsi.

Episode 74 | Kuzima kwa MTV

Kufuatia Paramount kuzifunga chaneli za MTV zilizokuwa zikipiga muziki pekee sehemu mbali mbali duniani, episode hii inakuletea makala fupi iliyolenga kukujuza kuhusu kuchipua, kukua, kubadilika na hatimaye kuporomoka kwa brand hii iliyoweka alama mioyoni mwa watu wengi.

Episode 73 | Consistency

Katika episode hii ya mwisho kwa mwaka 2025, host anapata nafasi ya kuzungumza na rafiki yake kuhusu alichojifunza ndani ya mwaka huo, kazi za sanaa alizozifurahia zaidi, matumizi ya AI na mengineyo.

Episode 72 | Little rooms

Kupitia hotuba ya Andre 3000 kwenye Rock n' roll hall of fame 2025, tunakumbushwa kwamba mafanikio mengi makubwa duniani huanzia kwenye vyumba vidogo sana (Little rooms).

Episode 71 | Netflix yazidi kutanua mbawa

Netflix yainunua Warner Bros. kwa bilioni za kimarekani 82.7. Hii inamaanisha nini kwenye kiwanda cha filamu duniani?

Episode 70| Makala ya Diddy

Episode hii inaangazia makala (Documentary) mpya iliyotolewa na 50 Cent kumuhusu hasimu wake Diddy.

Episode 69 | Hiphop vs Singeli

"Hiphop na Singeli ni aina mbili za muziki tofauti kabisa!" Sikiliza episode hii uone jinsi gani kauli hii inavyopoteza mashiko.

Episode 68 | Timbaland, why?

Pale mtayarishaji bora na gwiji wa muziki anapoamua kukumbatia teknolojia mpya katika muziki na kusahau haki na fursa ambazo teknolojia hiyo inazivunja na kunyima wasanii, nafasi yake inabakia wapi?
4 of 11