Wanangu podcast

Wanangu podcast

by Goodluck Joseph

Episode 7 | Rise and fall

Kupanda na kushuka.

Episode 6 | Fake it with me

Take care of home before impressing the street.

Episode 5 | Gifting

Fahamu njia zitakazokufanya uwe mtoaji zawadi mzuri.

Episode 4 | Parenting

Episode hii inahusu jukumu la malezi kwa watoto wetu.

Episode 3 | Generational myopia

Episode hii inaangazia umuhimu wa kutambua mchango wa kila kizazi, kilichopita, cha sasa na kijacho katika mwenendo mzima wa maisha.

Episode 2 | Reading

Katika episode hii unajadiliwa utaratibu wa kusoma vitabu mahususi kwa wale wanaotamani kuingia katika mtindo huu wa maisha.

Episode 1 | Tipping.

Episode hii inaangazia suala la utoaji tip. Je, huwa unatoa tip?

Episode 103 | Usichokimaliza Hukaa Akilini

Katika episode hii, Host anaangazia dhana ya kisaikolojia inayojulikana kama ‘The Zeigarnik Effect’, inayoeleza kwamba binadamu huwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukumbuka kazi au mambo ambayo bado hajayakamilisha kuliko yale ambayo tayari ameyamaliza. Kwa nini hali hii hutokea, na inaathirije maisha yetu ya kila siku? Karibu ufuatilie.

Episode 97 | Kunawa Mikono Haikuwa Kawaida ya Madaktari

Episode hii inaangazia maisha na mchango wa Ignaz Semmelweis, daktari wa karne ya 19 aliyegundua kwamba kunawa mikono kabla ya kuwahudumia wagonjwa kulipunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya wanawake waliokuwa wanajifungua. Licha ya ushahidi wake kuokoa maisha mengi, alipingwa na kudharauliwa na jamii ya kitabibu ya wakati wake kwa sababu mawazo yake yalikwenda kinyume na imani zilizokuwepo. Mwisho wake haukuwa mzuri.

Episode 75 | Mbuzi by Dizasta Vina (Uchambuzi)

Episode hii inahusu uchambuzi wa wimbo wa “Mbuzi” wa Dizasta Vina kutoka katika album yake ya A Father Figure (2024). Host anachambua Muundo, uandishi, dhamira kuu, mistari pendwa na mchango wa wimbo huu katika maisha yetu ya kila siku. Karibu!
11 of 11