

Usipuuze Maumivu ya Aliyejeruhiwa!
Episode notes
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 13:19–20 tunabaki katika simulizi ngumu ya Tamari.
Jana tuliona ukatili ambao Amnoni alimfanyia. Leo Biblia haitukimbizi haraka kwenda kwenye tukio jingine.
Inatuonyesha Tamari baada ya tukio.
Anararua vazi lake. Anaweka majivu kichwani. Anaweka mkono kichwani na anaondoka akilia.
Biblia haitufichi maumivu yake.
Na labda nasi hatupaswi kuyakimbia.
Wakati mwingine tunapokutana na mtu aliyeumia, tunakuwa na haraka ya kusema kitu. Tunataka kutoa explanation. Tunataka kumpa advice. Tunataka kumwambia, “Utakuwa sawa.” Au tunataka kupata lesson na kuendelea.
Lakini kuna wakati huduma ya kwanza si kusema.
Ni kusikiliza.
Ni kumpa nafasi mtu kueleza maumivu yake.
Ni kutomlaumu.
Ni kutompunguzia kile alichopitia.
Ni kuhakikisha yuko salama na anapata msaada anaohitaji.
Warumi 12:15 inasema:
“Lieni pamoja nao waliao.”
Wakati mwingine Biblia haituiti kwanza kueleza kwa nini mtu analia.
Inatuita kulia naye.
Na simulizi la Tamari linatupa challenge nyingine muhimu sana kwa familia zetu, makanisa yetu, workplaces na jamii zetu.
Mtu anapoumizwa na mtu mwenye nguvu au anayeheshimika, tunalinda nini kwanza?
Image ya familia? Reputation ya taasisi? Jina la mtu mwenye nguvu? Au usalama na utu wa aliyeumizwa?
Tusimfanye aliyeumia akae kimya ili sisi tuendelee kuonekana vizuri.
Tusimtwike aibu ambayo si yake.
Na tusifanye reputation ya taasisi kuwa muhimu kuliko usalama wa mtu.
Yesu alipokutana na watu waliokuwa wameumia, hakuwafanya kuwa interruptions. Aliwaona.
Na huenda hilo ndilo Neno letu leo:
Mwangalie aliyeumia.
Msikilize.
Mwamini pale inapofaa na chukua anachosema kwa uzito.
Msaidie kupata usalama na msaada anaohitaji.
Usikimbilie kumrekebisha wakati anahitaji kwanza kusikilizwa.
Kwa sababu wakati mwingine jambo kubwa zaidi unaloweza kumfanyia mtu aliyejeruhiwa si kuwa na jibu la maumivu yake.
Ni kuhakikisha habebi maumivu hayo akiwa peke yake.
Mungu anawaona wale ambao wengine wamewafanya wasionekane.
Na sisi pia tunaitwa kuwaona.
Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨