Kwa Jina la Bwana!
Neno la Leo by Neno la Leo 255
Episode notes
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:45 tunafika katika moja ya kauli zenye nguvu zaidi katika simulizi ya Daudi na Goliathi. Goliathi anasimama mbele ya Daudi akiwa na upanga, fumo, mkuki, uzoefu wa vita na mwonekano wa kutisha. Daudi ana fimbo, kombeo na mawe.
Kwa macho ya kibinadamu, hakuna ushindani.
Lakini Daudi anasema: “Wewe unanijia kwa upanga na fumo na mkuki, bali mimi ninakujia kwa jina la Bwana wa majeshi.”
Na hapo ndipo tunagundua siri ya ujasiri wa Daudi.
Haikuwa kombeo. Haikuwa jiwe. Wala haikuwa confidence kubwa ndani yake mwenyewe. Daudi alikuwa anajua Mungu anayesimama nyuma yake.
Hili ni muhimu sana kwa sababu tunaweza kuisoma simulizi ya Daudi na Goliathi kama motivational story inayosema, “Jiamini na unaweza kush ...Â