Utii ni Bora Kuliko Dhabihu!
Neno la Leo by Neno la Leo 255
Episode notes
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 15:22–23 tunafika katika moja ya nyakati muhimu sana katika maisha ya Sauli. Mungu alikuwa amempa agizo lakini Sauli hakulitekeleza kikamilifu. Alipoulizwa kwa nini, akatoa sababu iliyosikika ya kiroho: baadhi ya vitu vilihifadhiwa ili vitolewe sadaka kwa Bwana. Ndipo Samweli akasema maneno ambayo yameendelea kutukumbusha mpaka leo: “Kutii ni bora kuliko dhabihu.”
Tatizo la Sauli halikuwa kwamba hakumtii Mungu kabisa. Alitii sehemu ya agizo na akaacha sehemu ambayo haikumfaa. Kisha akajaribu kutumia jambo la kidini kuhalalisha kile ambacho Mungu hakumwagiza.
Na hapo ndipo Neno la leo linapotufikia sisi pia. Je, inawezekana nasi tukawa tunamtii Mungu kwa masharti yetu? Tunaweza kwenda kanisani, kuomba, kutoa sadaka, kusoma ...Â