UNAHITAJI WIKI MBILI TU ILI KUBADILISHA MAISHA YAKO
Je, kweli maisha yanaweza kubadilika ndani ya wiki mbili? Katika episode hii ya kwanza, tunazungumzia kwa nini watu wengi hushindwa kubadilika si kwa sababu hawana uwezo, bali kwa sababu hawadumu kwenye hatua mpya kwa muda wa kutosha. Utajifunza jinsi tabia ndogo za kila siku zinavyoanza kuijenga akili yako, kuunda utambulisho mpya, na kuweka msingi wa mabadiliko makubwa ya muda mrefu. Hii si ahadi ya miujiza. Ni mazungumzo kuhusu nguvu ya consistency, nidhamu, na kuamua kuanza leo badala ya kusubiri siku na wakati sahihi. Ukimaliza kusikiliza episode hii, utakuwa na mtazamo mpya kuhusu: Kwa nini siku 14 zinaweza kuwa mwanzo wa maisha mapya. Jinsi ya kuacha kuahirisha mabadiliko. Hatua rahisi za kuanza kujenga tabia zinazokusogeza mbele kila siku. Kama unapenda maudhui ya mindset, nidhamu, maendeleo binafsi na kujenga maisha bora, hakikisha umefollow podcast hii ili usikose episode zinazofuata. Safari ya kujibadilisha inaanza leo.