Wanangu podcast

Wanangu podcast

di Goodluck Joseph

Episode 57 | Marion Stokes

Kutana na Marion Stokes mmarekani aliyekuwa akirekodi vipindi vya televisheni nyumbani kwake masaa 24 kila siku kwa miaka 35 mfululizo.

Episode 56 | Makoma

Fuatilia kuinuka, kupaa, kuanguka, na kunyanyuka tena kwa moja kati ya makundi bora na muhimu ya muziki wa injili kuwahi kutokea barani Afrika.

Episode 55 | Pretty privilege

Baada ya likizo isiyokuwa rasmi, host anarejea na 'Pretty privilege', episode iliyojikita katika kudadavua maana ya dhana inayodai kwamba watu wenye mvuto au uzuri hupendelewa katika nyanja mbali mbali za kimaisha. Karibu!

Episode 54 | Chinese bamboo

Katika kipindi hiki, unatumika mfano wa mianzi ya kichina (Chinese bamboo) na jinsi inavyotufundisha uvumilivu, ustahimilivu, na imani katika maisha. Kama mimea hii, inavyochukua muda mrefu bila kuonyesha dalili zozote za ukuaji kabla ya kukua ghafla kwa kasi, juhudi zetu pia mara nyingi huchukua muda kuzaa matunda.

Episode 53 | Nadharia ya njama

Fahamu maana halisi ya 'Nadharia ya Njama' (Conspiracy theory) na chunguza kwa undani sababu zinazowafanya watu kuvutiwa au kuamini juu ya nadharia hizo. Host wako anakupa mtazamo mpana na mifano halisi kuhusiana na jinsi gani nadharia hizi huenea na kupokelewa kwa urahisi katika jamii.

Episode 52 | Umesikia kuhusu vibe coding?

Akili bandia inazidi kutuonyesha kwamba haijaja kucheza na sisi. Sikiliza jinsi unavyoweza kutengeneza software bila utaalamu wowote, kinachotakiwa ni vibe yako tu!

Episode 51 | Sakata la Luigi Mangione (Part 2)

Episode hii ni mwendelezo (part 2) wa episode 48 kuhusu kisa cha Luigi Mangione (26) anayeshitakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa CEO wa kampuni ya bima ya afya nchini marekani, Brian Thompson.

Episode 50 | 'The ICU is the ICU.'

Kama binadamu tunajifunza kupitia mambo mengi, sikia funzo hili ambalo host amelipata wakati akirudia kuangalia series ya Succession.

Episode 49 | Overconfidence

Katika episode hii host anazungumza kuhusu hali ya kujiamini kupita kiasi (Overconfidence). Kwa kutumia mifano, anafafanua mazingira ambayo tabia hii huweza kujitokeza katika maisha yetu ya kila siku pengine mara nyingi kuliko wengi tunavyodhani.

Episode 48 | Sakata la Luigi Mangione

Fuatilia kesi ya kijana Luigi Mangione anayeshutumiwa kwa kosa la kumuua kwa kumpiga risasi CEO wa shirika binafsi la bima ya afya nchini marekani bwana Brian Thompson.
6 di 11