Wanangu podcast

Wanangu podcast

di Goodluck Joseph

Episode 67 | Sauti Sol

Safari ya Sauti Sol katika muziki, kuanzia kuundwa kwa bendi, kazi walizofanya na hatimaye kuvunjika.

Episode 66 | Camp Mulla: Jiwe walilokataa waashi.

Fuatilia hadithi ya namna Camp Mulla ilivyokuja kuwa moja ya makundi ya muziki ambayo hayatasahaulika kwa miaka mingi ijayo.

Episode 65 | Je, Ayesha Curry hana shukrani?

Katika ulimwengu huu uliyojaa maoni ya kila namna kupitia mitandao ya kijamii, pale mke wa moja ya nyota wa mpira wa kikapu duniani anapoitwa asiye mwenye shukrani, kuna lipi la kujifunza?

Episode 64 | Viashiria vinapogeuka mtego

Je, viashiria vinapogeuka kuwa malengo, bado vinaonyesha hali halisi? Jua kwanini mara nyingi namba hazielezi ukweli wote. Sikiliza namna ya kutambua mtego wa viashiria katika maisha ya kila siku.

Episode 63 | Charlie Kirk

Katika episode hii host anazungumzia mauaji ya mwanaharakati Charlie Kirk aliyepigwa risasi mnamo tarehe 10 septemba, 2025 huko Utah nchini marekani. Yapi hasa yalikuwa ni maisha aliyoishi enzi za uhai wake, na ni itikadi zipi alizozisimamia zilizosababisha kutokea kwa mauaji hayo? Tega sikio.

Episode 62 | Sanaa ya kuachilia

Katika maisha, mara nyingi tunafundishwa kujifunza mambo mapya, lakini wachache hufundishwa kuachilia yale yasiyotufaa tena. Katika kipindi hiki tunazungumzia sanaa ya kuachilia, yaani uwezo wa kuacha imani, mitazamo, na mazoea yaliyopitwa na wakati ili kufungua nafasi ya ukuaji mpya.

Episode 61 | Vua gamba

Kambakoche anaweza kutufundisha nini kuhusu maisha? Katika kipindi hiki tunaangazia ukweli kwamba mara nyingine shinikizo katika maisha ni ishara ya kukua.

Episode 60 | Usiendeshwe na matokeo

Kumbe matokeo ya mitihani huathiri maisha sio tu ya wale waliofanya vibaya bali hata waliofaulu vizuri. Katika episode hii host anatumia hadithi ya kweli kufikisha ujumbe huo. Pia, pata kusikia kuhusu segment mpya iliyoongezeka kwenye show. Karibu!

Episode 59 | Kwanini chenji ni tatizo Tanzania?

Kwa nini kupata chenji baada ya kununua kitu ni tatizo nchini Tanzania? Katika episode hii host anajadili sababu, madhara na suluhisho la kadhia hii.

Episode 58 | AGI: The dinosaurs of AI

Kuna uhusiano gani kati ya dinosaurs (Mijusi mikubwa ya kale) na Akili bandia? Katika episode hii, host anazungumzia maana halisi ya AGI, historia yake, maoni ya wataalamu, na kwa nini mustakabali wake unaweza kuwa muhimu, wenye kutisha na usiotabirika.
5 di 11