Upendo wa Kweli Huheshimu Mipaka!...

Upendo wa Kweli Huheshimu Mipaka!

IA
Neno la Leo di Neno la Leo 255
S4 · E6
6 ott 2026
09:30

Note sull'episodio

🎙️ Leo katika Neno la Leo tunatafakari 2 Samweli 13:10–14, sehemu nzito na yenye maumivu katika simulizi la familia ya Daudi.

Amnoni anapokuwa peke yake na Tamari anajaribu kumlazimisha kutimiza tamaa yake. Tamari anakataa wazi. Anasema, “Usifanye jambo hili.”

Lakini Amnoni hasikilizi.

Anatumia nguvu zake na kumdhuru.

Hapa Biblia inatuweka mbele ya ukweli ambao hatupaswi kuuficha kwa lugha nyepesi:

Tamari alisema hapana. Amnoni hakuheshimu hapana yake.

Huo haukuwa upendo.

Upendo wa kweli haumfanyi mwingine kuwa chombo cha kutimiza tamaa zetu. Upendo haupimi tu kile tunachotaka sisi. Unaheshimu utu, sauti na mipaka ya mwingine.

Ndiyo maana 1 Wakorintho 13:5 inasema kwamba upendo “hautafuti mambo yake.”

Na tunapoisoma simulizi hii ni muhimu tusimwangalie Amnoni pekee. Tumwone Tamari pia.

Hakusababisha alichofanyiwa.

Alisema hapana.

Alijaribu kumzuia.

Responsibility ilikuwa ya Amnoni ambaye alichagua kupuuza sauti yake na kutumia nguvu dhidi yake.

Hili ni muhimu sana hata katika mahusiano yetu leo.

Kuwa katika relationship hakumpi mtu ownership ya mwili wa mwingine. Ndoa, uchumba au ukaribu hauondoi umuhimu wa kuheshimiana. Upendo wa kweli hauulizi tu, “Mimi nataka nini?” Unauliza pia, “Je, ninamheshimu huyu mtu?”

Na kwa wale wanaobeba maumivu ya kudhulumiwa, simulizi la Tamari linatukumbusha kwamba aibu haipaswi kuwekwa juu ya aliyedhulumiwa. Responsibility ni ya aliyefanya ukatili.

Upendo wa kweli unasikiliza. Upendo wa kweli haukulazimishi. Upendo wa kweli unaheshimu “hapana.”

Karibu katika Neno la Leo tunapotafakari somo hili muhimu na kuomba Mungu atufundishe kuwapenda wengine kwa heshima, utu na moyo usiotafuta faida yake mwenyewe.