Mungu Anaweza Kukurejeshea Ulicho...

Mungu Anaweza Kukurejeshea Ulichofikiri Kimepotea!

IA
Neno la Leo di Neno la Leo 255
S3 · E60
29 set 2026
15:58

Note sull'episodio

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 30:8, 18–19 tunaendelea na Daudi baada ya moja ya siku ngumu zaidi katika maisha yake.

Jana tulimwacha Ziklagi ikiwa imechomwa moto. Familia zimechukuliwa mateka. Watu wake wamevunjika moyo kiasi cha kutaka kumpiga mawe.

Daudi akalia mpaka hakuwa na nguvu tena za kulia.

Lakini Biblia ikasema:

“Daudi akajitia nguvu katika Bwana Mungu wake.”

Leo tunaona jambo muhimu sana. Baada ya kupata nguvu, Daudi hafanyi maamuzi kwa hasira. Hakimbilii kuwafukuza Waamaleki kwa sababu tu anajua kupigana.

Anafanya kitu ambacho tumemwona akikifanya kabla:

Anamwuliza Mungu.

“Je, nikiwafuata nitawapata?”

Hili ni muhimu. Maumivu hayakumfanya Daudi aache kutafuta mwongozo wa Mungu. Hata baada ya kila kitu kilichotokea, bado anarudi kwenye swali lilelile:

“Bwana, nifanye nini sasa?”

Mungu anamwambia afuatilie. Daudi anachukua hatua na mwisho Biblia inasema:

“Daudi akavipata vyote.”

Jana alikuwa analia akitazama kile alichofikiri amepoteza. Leo anashuhudia kurejeshwa kwake.

Lakini hapa tunahitaji kuelewa ujumbe huu vizuri.

Biblia haitufundishi kwamba kila kitu tunachopoteza katika maisha lazima kirudi exactly katika namna ileile. Kuna hasara ambazo ni halisi. Kuna milango inayofungwa. Kuna vipindi vinavyokwisha na kuna mambo ambayo hayatakuwa tena kama yalivyokuwa.

Lakini Ziklagi inatufundisha jambo jingine lenye nguvu:

Hasara haimaanishi kwamba Mungu amemaliza hadithi yako.

Daudi alipokuwa analia hakujua kwamba recovery ilikuwa mbele yake.

Na huenda nasi tunafanya kosa la kuweka full stop katika sehemu ambayo Mungu ameweka comma.

Tunasema, “Imeisha.”

Mungu bado anaandika.

Tunasema, “Hakuna kitakachotokea tena.”

Lakini hatujaiona kesho.

Restoration yako inaweza isifanane exactly na kile kilichopotea. Inaweza kuwa Mungu kurejesha nafasi. Inaweza kuwa uponyaji wa moyo. Inaweza kuwa direction mpya. Inaweza kuwa hekima uliyoipata kupitia kile ulichopitia au mwanzo mpya ambao hukuwahi kuufikiria.

Jambo muhimu ni hili: usifanye maumivu ya jana kuwa unabii wa kesho yako.

Angalia journey ya Daudi:

Alilia. Akajitia nguvu katika Bwana. Akamwuliza Mungu. Akasikia direction. Kisha akasimama na kwenda.

Hiyo ndiyo faith journey.

Kuna wakati wa kulia. Kuna wakati wa kujitia nguvu katika Mungu. Kuna wakati wa kuuliza, “Bwana, hatua inayofuata ni ipi?”

Halafu kuna wakati wa kusimama na kwenda.

Kwa hiyo kama leo unasimama mbele ya Ziklagi yako na kuona majivu ya kitu ulichokipenda, usikimbilie kuamua kwamba kila kitu kimekwisha.

Usiweke full stop mahali Mungu bado anaandika.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨