The Life Through My Lenses Podcast

The Life Through My Lenses Podcast

di Tulinave
Stagione 1

EP 03: From School To Reality

Katika safari ya mafanikio, sehemu kubwa ya maandalizi yetu huanzia shuleni. Katika episode hii, nitaongelea mtazamo na uhalisia wa mafanikio, kuanzia mtu akiwa shuleni hadi anapofika kwenye utu uzima. Nimeongelea experience yangu katika shule niliyosoma, pamoja na observations zangu kuhusu maisha yangu na baadhi ya classmates wangu kwa ujumla. I dedicate this episode to SMSS Class of 2014. Karibu usikilize.

EP 02: MASHAURI KUHUSU NDOA

Hi, episode hii ni kwa kila binti aliye kwenye umri wa kukaribia kuolewa au anayetamani kuolewa. Kuna wimbi kubwa la ushauri kutoka kwa watu tofauti, wanawake walioolewa, wanawake wakubwa, viongozi wa dini, mitandao ya kijamii na watu wenye mitazamo mbalimbali kuhusu ndoa. Kila mmoja ana mtazamo wake, na wakati mwingine One issue kwenye ndoa inaweza kuwa na Different advice depending on who you ask!!!.... Sasa, wewe kama binti, unajiuliza nimsikikize nani? Katika episode hii, kupitia mtazamo wangu, nazungumzia namna tunavyoweza kuupokea na kuuchuja ushauri huu bila kupoteza tunachotaka sisi wenyewe, huku tukiendelea kuwa na heshima kwa waliotuzidi umri na uzoefu. Na kwa wale wanaotoa ushauri, hasa wanawake walio kwenye ndoa au wenye uzoefu, naamini episode hii itawasaidia kutambua pia mtazamo na changamoto ambazo watoto, wadogo au mabinti walio karibu nao wanakutana nazo. Karibu usikilize hadi mwisho.

Ep01: MWANZO MZURI- From Talking to Myself to Talking to You

Karibu kwenye show yangu. Nitakuwa nikizungumzia mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii yetu—familia, mahusiano, maisha na mada nyingine zinazogusa maisha yangu na yetu kwa ujumla. Hapa natoa mtazamo wangu, lakini pia naamini kila mtu ana haki ya kuwa na mtazamo wake. Naamini katika maongezi yenye kusikiliza na kubadilishana mawazo bila kudharauliana wala kukandamizana. Na zaidi ya yote, napenda kucheka, kufurahi na kupiga story. So, let's talk about anything.