Usingoje Kila Mtu Aamini Ndipo Wewe Uamini!
Neno la Leo di Neno la Leo 255
Note sull'episodio
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:32 tunafunga wiki yetu ya kwanza ya Septemba tukiwa tumemfuata Daudi kutoka malishoni mpaka sasa amesimama mbele ya mfalme.
Kwa siku nyingi jeshi la Israeli limekuwa likimsikiliza Goliathi akitoa vitisho. Kila anapotokea, hofu inaenea. Wanaume waliofunzwa vita wanaona ukubwa wa tatizo na mioyo yao inakata tamaa. Lakini Daudi, kijana ambaye hata hakuwa mwanajeshi, anafika mbele ya Sauli na kusema, “Moyo wa mtu yeyote usizimie kwa ajili yake. Mtumishi wako atakwenda kupigana na huyu Mfilisti.”
Mazingira hayajabadilika. Goliathi bado yupo. Jeshi la Wafilisti bado lipo. Kilichobadilika ni kwamba sasa kuna mtu mmoja ambaye amekataa kuiona hali kupitia hofu ya kila mtu mwingine.
Neno la leo linatufundisha kwamba tunapa ...