Usiruhusu Maneno ya Watu Yazuie Kufikia Malengo Yako!
Neno la Leo di Neno la Leo 255
Note sull'episodio
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:28–29 tunaendelea na simulizi ya Daudi na Goliathi. Jana tuliona Daudi akiitazama changamoto kwa macho tofauti. Lakini kabla hajafika hata mbele ya Goliathi, anakutana na vita nyingine ambayo huenda hakuitarajia: maneno ya ndugu yake mwenyewe, Eliabu.
Eliabu anamsikia Daudi akiuliza kuhusu Goliathi, anakasirika na kuanza kumshutumu. Anahoji sababu ya Daudi kuja vitani na hata kutafsiri vibaya nia ya moyo wake.
Fikiria hilo: Daudi hajapigana na Goliathi lakini tayari kuna mtu anayemwambia, kwa namna fulani, “Wewe unafanya nini hapa?”
Na maisha yanaweza kuwa hivyo pia. Kabla hujafika kwenye changamoto yenyewe unaweza kukutana na sauti zinazokuambia huwezi, hujui, huna uzoefu, hufai au hata kwamba nia yako si nzuri. ...