MWANAHISABATI

MWANAHISABATI

di Arthur Geil
NINI KITATOKEA KABLA YA KUYAFIKIA MAFANIKIO YAKO!
NINI KITATOKEA KABLA YA KUYAFIKIA MAFANIKIO YAKO? 🎙️ Kabla hujafika kwenye maisha unayoyaota, kuna kipindi ambacho utajiuliza kama kweli uko kwenye njia sahihi. Utakutana na rejection. Utapoteza pesa. Utapoteza watu. Utaona wengine wanakupita. Utafanya kazi bila kuona matokeo. Na kuna muda utaanza kujiuliza kama kweli unaweza. Tatizo ni kwamba, wengi huchukulia temporary defeat kama permanent failure. Wanashindwa mara chache, wanaona wamefeli. Wanajaribu biashara, haifanyi vizuri, wanaacha. Wanaanza kujenga kitu, hawapati attention, wanakata tamaa. Wanapitia kipindi kigumu, wanaamini maisha yamewaambia “hii sio njia yako.” Lakini vipi kama hicho kipindi hakijaja kukuambia uache? Vipi kama kimekuja kukufundisha, kukujenga na kukuandaa kwa kile unachokisaka? Katika episode hii tunazungumzia mambo ambayo yanaweza kutokea kabla hujafikia mafanikio yako, kwa nini kushindwa hakumaanishi safari imeisha, na kwa nini unatakiwa kujifunza kuanza tena unapopigwa na maisha. 🎧 NINI KITATOKEA KABLA YA KUYAFIKIA MAFANIKIO YAKO! Sikiliza episode hii mpaka mwisho. Na ukumbuke: Temporary defeat si mwisho wa safari. — MWANAHISABATI Arthur Geil
UNAHITAJI WIKI MBILI TU ILI KUBADILISHA MAISHA YAKO
Je, kweli maisha yanaweza kubadilika ndani ya wiki mbili? Katika episode hii ya kwanza, tunazungumzia kwa nini watu wengi hushindwa kubadilika si kwa sababu hawana uwezo, bali kwa sababu hawadumu kwenye hatua mpya kwa muda wa kutosha. Utajifunza jinsi tabia ndogo za kila siku zinavyoanza kuijenga akili yako, kuunda utambulisho mpya, na kuweka msingi wa mabadiliko makubwa ya muda mrefu. Hii si ahadi ya miujiza. Ni mazungumzo kuhusu nguvu ya consistency, nidhamu, na kuamua kuanza leo badala ya kusubiri siku na wakati sahihi. Ukimaliza kusikiliza episode hii, utakuwa na mtazamo mpya kuhusu: Kwa nini siku 14 zinaweza kuwa mwanzo wa maisha mapya. Jinsi ya kuacha kuahirisha mabadiliko. Hatua rahisi za kuanza kujenga tabia zinazokusogeza mbele kila siku. Kama unapenda maudhui ya mindset, nidhamu, maendeleo binafsi na kujenga maisha bora, hakikisha umefollow podcast hii ili usikose episode zinazofuata. Safari ya kujibadilisha inaanza leo.