Unaweza Kufanikiwa Bila Kumpoteza...
IA
Unaweza Kufanikiwa Bila Kumpoteza Mungu Njiani!
IA

Neno la Leo di Neno la Leo 255

Note sull'episodio

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 18:14 tunakutana na maneno machache lakini yenye ujumbe mkubwa sana kuhusu maisha ya Daudi: “Daudi akafanikiwa katika njia zake zote, naye Bwana alikuwa pamoja naye.”

Ni rahisi kusimama kwenye sehemu ya kwanza, “Daudi akafanikiwa.” Lakini siri ya maisha yake ipo katika sehemu inayofuata: “Bwana alikuwa pamoja naye.”

Mwezi huu tumemfuata Daudi kutoka malishoni. Tulimwona akiwa kijana asiyepewa nafasi kubwa hata ndani ya familia yake. Akaingia ikulu. Akasimama mbele ya Goliathi. Akapata ushindi na jina lake likaanza kujulikana katika Israeli. Sasa Sauli anaanza kumwonea wivu na kumwangalia kwa mashaka.

Mazingira ya Daudi yanaendelea kubadilika lakini uwepo wa Mungu unabaki kuwa msingi wake. ... 

Leggi dettagli