Usijaribu Kuwa Mtu Mwingine!
Neno la Leo di Neno la Leo 255
Note sull'episodio
ποΈ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:38β40 tunaendelea na simulizi ya Daudi kuelekea kwa Goliathi. Baada ya Sauli kukubali Daudi aende kupigana, anamvika mavazi yake ya vita, kofia ya shaba, deraya na kumpa upanga. Ni vifaa vizuri kabisa vya vita, lakini Daudi anapojaribu kutembea navyo anatambua jambo muhimu: hajavizoea.
Anavivua.
Badala yake anachukua fimbo yake, mawe matano laini na kombeo lake, vitu ambavyo alikuwa amejifunza kuvitumia muda mrefu akiwa malishoni.
Neno la leo linatukumbusha kwamba si kila kitu kinachomfaa mtu mwingine kitakufaa wewe. Tunaweza kujifunza kutoka kwa watu, kupokea ushauri, mentorship na maarifa yao lakini hatuhitaji kuwa nakala zao.
Mara nyingi tunapokaribia nafasi kubwa tunaanza kuangalia waliofanikiwa kabla yΒ ...Β