Wanangu podcast

Wanangu podcast

por Goodluck Joseph

Episode 110 | Tunafuata Muziki au Tunatafuta Likes?

Katika episode hii, host anaibua swali: je, kadri tunavyozidi kwenda mbele, mashabiki wanapoteza uhusiano wao wa moja kwa moja na muziki na kuanza kujali zaidi vitu vinavyouzunguka, kama vile ‘likes’ na engagement kwenye majukwaa ya usambazaji wa muziki kama YouTube? Akiendelea kuchunguza sababu zinazoweza kuwa nyuma ya mabadiliko haya, host anarudisha ‘mic’ kwako na kukuuliza: wewe unaonaje kuhusu hili?

Episode 109 | Malengo Yanavyoweza Kukupoteza

Katika episode hii, Host anatoka nje ya box na kukuletea wazo linalokwenda kinyume na matarajio ya wengi: kwamba kama unataka kufanikiwa zaidi katika unachokifanya, huenda ukahitaji kuacha kuwa na malengo. Akirejea kwenye kitabu kilichomtambulisha wazo hili, Host anaeleza kwa nini mfumo wa maisha unaotufundisha kuweka malengo unaweza kuwa na mapungufu yake. Lakini hoja hapa si kwamba tusiwe na malengo kabisa, bali ni kutambua kwamba wakati mwingine malengo hututoa kwenye reli.

Episode 108 | Fikra Sahihi Huja Kwa Lugha Asili

Fuatilia jinsi mstari mmoja wa Nash Mc unavyoweza kuzalisha maswali mengi na yenye kutafakarisha kuhusu uhusiano na kutegemeana kati ya lugha na fikra. Ni kama hadithi ya nani alianza kati ya yai na kuku, lakini safari hii ikiwa katika uwanja wa lugha na utambuzi. Je, lugha ndiyo huchochea namna tunavyofikiri, au fikra ndizo huunda lugha tunayotumia?

Episode 107 | A.k.a Mimi by Ngwair (Uchambuzi)

Katika episode hii, Host anaichambua album ya kwanza ya Ngwair, A.K.A Mimi, na kueleza mambo aliyogundua baada ya kuisikiliza tena akiwa mtu mzima. Wakati album hii ilipotoka, alikuwa bado mdogo na huenda hakuwa na uwezo wa kuielewa kwa kina kama anavyoweza leo. Safari hii, anaisikiliza kwa mtazamo tofauti; akiunganisha “dots” zilizopo baina ya nyimbo, mambo yanayofanya album hii isimame kama kazi moja yenye mshikamano wa dhamira, ujumbe na ubunifu, pamoja na vipengele vingine ambavyo huenda vilimpita wakati huo. Ugunduzi huo unamfanya aeleze kwa nini anaamini A.K.A Mimi ni album yenye uzito, kina na ubora mkubwa kuliko wengi wanavyoweza kudhani.

Episode 106 | Usiamini Hadithi Moja Tu

Katika episode hii, tunaangazia tabia ya kuchukua hadithi ya mtu mmoja na kuitumia kama ushahidi wa kuhitimisha jambo kubwa zaidi. Kupitia mifano ya maisha ya kila siku, katika afya, biashara na social media, tunaona jinsi kauli kama “Mimi ninamjua mtu ambaye…” zinavyoweza kutufanya tufanye maamuzi yasiyo sahihi. Episode hii inatukumbusha kwamba stori moja inaweza kuwa ya kweli, lakini isiwe ushahidi wa kutosha kueleza picha nzima, na kwamba tunapaswa kujifunza kutofautisha kati ya hadithi ya mtu binafsi na ushahidi uliotokana na uchunguzi kabla ya kufikia hitimisho.

Episode 105 | Kampuni Inayouza Rangi Bila Kuuza Rangi!

Katika Episode hii, tunaangazia historia ya kuvutia ya Pantone, mfumo uliobadilisha namna dunia inavyotambua, kuwasiliana na kutumia rangi. Tutafuatilia jinsi wazo la kuunda mfumo wa kutambua rangi lilivyoanza, namna Pantone ilivyogeuka kutoka kwenye mfumo wa kawaida wa kuchanganua rangi na kuwa sehemu muhimu ya ulimwengu wa ubunifu, mitindo, matangazo na biashara. Karibu!

Filamu ya Afrika Iliyowahamasisha Jay-Z na Beyoncé

Je, ni nini kinachofanya filamu iliyotengenezwa Afrika zaidi ya miaka 50 iliyopita iendelee kuzungumziwa, kupongezwa na hata kuwavutia mastaa kama Jay-Z na Beyoncé? Katika episode hii, host anasimulia Touki Bouki, mojawapo ya filamu kubwa na zenye ushawishi kuwahi kutokea Afrika. Tunafuatilia safari ya wahusika Mory na Anta, lakini zaidi ya hapo, tunaangalia kile ambacho filamu hii inakisema kuhusu Afrika, ndoto za kuondoka, utambulisho, mapenzi na tamaa ya maisha bora. Kwa nini Touki Bouki imeendelea kuwa muhimu kwa vizazi tofauti vya Waafrika? Na ilikuwaje filamu hii ya Senegal ikawafikia na kuwavutia Jay-Z na Beyoncé? Karibu!

Kupenda Kwangu 'Titles' Kunanigharimu

Katika episode hii, host anakukaribisha ndani ya mawazo yake na kukuonyesha mchakato halisi anaoupitia kila anapotafuta title ya episode mpya. Ni safari iliyojaa vita ya ndani kati ya kuandika title inayomridhisha yeye kama ‘mbunifu’ na ile inayopewa kipaumbele na mtandao (algorithms) ili kuwafikia watu wengi zaidi. Anaeleza mapenzi yake ya muda mrefu juu ya titles nzuri tangu akiwa mtoto, hadi changamoto za zama za leo ambapo algorithms zinaonekana kuamua kinachofanya title iwe ‘nzuri’. Episode hii inaibua swali muhimu, Je, ubunifu unapaswa kuongozwa na maono ya mbunifu au na algorithm? Karibu katika mazungumzo haya ya ubunifu na mchakato wa kutafuta title nzuri.

Episode 101 | Timamu Kati ya Wasio Timamu

Katika episode hii, host anachambua utafiti maarufu uliofanywa na Dkt. David Rosenhan mwaka 1973, uliouliza swali muhimu kuhusu uwezo wa wataalamu wa afya ya akili kutofautisha kati ya mtu mwenye ugonjwa wa akili na anayejifanya kuwa nao. Matokeo ya utafiti huo yaliibua mjadala mkubwa na kuonyesha mapungufu yaliyokuwepo katika mfumo wa utambuzi wa magonjwa ya akili, kiasi cha kuwafanya wengi kuhoji usahihi wa baadhi ya uchunguzi wa kitabibu. Fuatilia simulizi hii ya kusisimua ili kujua Rosenhan alifanyaje utafiti huo na kwa nini hitimisho lake lilibadilisha mjadala kuhusu afya ya akili duniani.

Episode 100 | Kwanini Iliitwa Wanangu Podcast?

Host anaadhimisha kwa furaha kufikiwa kwa episode ya 100 ya Wanangu Podcast, akitoa shukrani za dhati kwa kila aliyekuwa sehemu ya safari hii, kuanzia wasikilizaji / watazamaji hadi marafiki waliotoa mawazo, ushauri na mchango wao katika kuiboresha podcast hii. Katika mazungumzo hayo, anasimulia pia chanzo cha jina Wanangu Podcast, sababu zilizomfanya alichague, na anagusia mafunzo makubwa aliyojifunza katika kipindi chote cha kuandaa na kuendesha podcast hii.
1 de 11