Usimzoee Mungu Mpaka Ukasahau Uta...
IA
Usimzoee Mungu Mpaka Ukasahau Utakatifu Wake!
IA

Neno la Leo por Neno la Leo 255

Notas del episodio

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 6:20 tunakutana na swali zito: “Ni nani awezaye kusimama mbele za Bwana, huyu Mungu mtakatifu?” Baada ya kuona jinsi Mungu alivyoonyesha nguvu zake dhidi ya Wafilisti, sasa Waisraeli wanakumbushwa kwamba Mungu si mwenye nguvu tu, Yeye ni mtakatifu. Neno la leo linatukumbusha kwamba tunaweza kumzoea Mungu kiasi cha kupoteza kicho na heshima tunayopaswa kuwa nayo mbele zake. Ni kweli Mungu ni Baba yetu na anatupenda lakini neema yake haijafanya dhambi kuwa jambo dogo wala utakatifu wake kupungua. Je, ukaribu wetu na Mungu umetufanya tumheshimu zaidi au tumemzoea kiasi kwamba mambo yake matakatifu yamekuwa ya kawaida kwetu? Mungu anatualika kuwa karibu naye lakini pia kutembea mbele zake kwa heshima, utiifu na utakatifu. ... 

Leer más