Fanya Unachoweza, Mungu Atashughulikia Usichoweza!
Neno la Leo por Neno la Leo 255
Notas del episodio
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:47 tunaendelea pale tulipoishia jana. Daudi amemwambia Goliathi, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Sasa anaongeza jambo muhimu zaidi: “Vita ni vya Bwana.”
Lakini angalia jambo hili. Baada ya kusema vita ni vya Bwana, Daudi hakukaa chini akisubiri Mungu afanye kila kitu. Bado alikimbia kuelekea kwa Goliathi. Bado alichukua jiwe. Bado alitumia kombeo lake.
Kwa hiyo kusema “vita ni vya Bwana” hakumaanishi kwamba hatuna sehemu ya kufanya. Inamaanisha tunajua tofauti kati ya wajibu wetu na kile ambacho ni Mungu pekee anaweza kufanya.
Na hapo ndipo Neno la leo linapotugusa. Tunaweza kufanya kila tunachoweza kwa ajili ya familia zetu lakini hatuwezi kudhibiti moyo wa kila mtu. Tunaweza kuf ...Â